-->

Mzee Majuto Afungukia Kuacha Kuigiza, Amrudia Mungu

Mzee majuto ambaye amejipatia umaarufu sana kwa uigizaji hususani katika Comedy ametoa kauli rasmi kuwa kwa sasa ameamua kuachana na kazi hiyo ya uigizaji na sasa kumtumikia Mungu na kuomba asamehewe makosa kwa yale aliyotenda nyuma.

MAJUTO22

Mzee Majuto amesema kuwa kwa sasa anaamini anaweza kuishi bila kutumia kipaji chake hicho cha ugizaji na muda huu atatumia kumuomba Mungu amasamehe makosa aliyotenda na kudai kuwa anaamini itawezekana kwani Mungu ndiye anayetoa ridhiki kwa kila mtu.

“Mashabiki zangu nawaomba wawe na amani tu kwa maamuzi yangu haya kwani hakuna kitu ambacho kinaishi milele kwani ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuishi milele, imefika wakati nimeamua kumpuzika na kumtumikia Mungu, naamini maisha yatakwenda kwani kuna watu ambao hawana vipaji ila wanaishi vyema, wanatibiwa na maisha yao yanakwenda salama hivyo hata mimi nitaishi vyema’ alisema Mzee Majuto.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364