-->

Mzee Majuto Atangaza Tena Kuacha Sanaa (Video)

Mchekeshaji na Muigizaji maarufu wa filamu nchini Tanzania, Alhaji Amri Athumani almaarufu Mzee Majuto ametangaza rasmi kustaafu kazi hiyo baada ya kuitumikia kwa zaidi ya ,miaka 30.

Mzee Majuto amesema amechukua maamuzi hayo baada ya kuona umri unaenda na uwingi wa changamoto wa kazi hiyo hivyo ameamua arudi kwenye kilimo na kumtumikia Mungu.

“Kwa sasa hivi mimi sanaa basi , nasema kwa kweli sanaa basi labda kutokee mtu anahitaji nimfanyie tangazo lake nikimaliza narudi shambani kwangu nimtumikie mwenyezi Mungu nimuombe toba kwa sababu tuliofanya ni mengi na kuna mazuri na mabaya na mabaya ndiyo yanayotawala kwenye maisha ya ujana kwa hiyo tumuombe toka Mwenyezi Mungu, kwani wakati ndiyo huu ukisema upange siku kila siku utapanga”,amesema Mzee Majuto kwenye mahojiano yake na gazeti la Habari Leo.

Licha ya kustaafu Mzee Majuto ameishauri serikali ijenge kambi nyingi za JKT ili kupunguza idadi ya vijana wanaokaa bila kazi mitaani.


Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364