-->

Sina Tabia Kutoka na Vijana Wadogo -Snura

snura-1Msanii wa muziki wa bongo fleva na filamu nchini Snura Mushi amefunguka na kusema kuwa yeye hana tabia ya kutoka kimapenzi na watoto wadogo kama baadhi ya wasanii wengine wa kike au watu maarufu wanavyofanya.

Snura alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ ya EATV na kudai aliweza kumkiss Raymond wakati anatengeneza video ya wimbo wake ‘Natafuta kiki’ kwani pale alikuwa kazini ila siyo kusema anatoka kimapenzi na msanii huyo kama ambavyo baadhi ya watu walivyoanza kuzusha anatoka naye baada ya kuona picha akimkiss Raymond.

“Baada tu ya kutoka ile picha mimi na RayVany tuki ‘kiss’ watu wakaanza kuniandika vibaya kwenye mitandao ya jamii, sijui RayVany ndiyo mwanaume aliyekuwa anamnyima usingizi Snura jamnii Raymond yule mimi ni mdogo wangu. Nili mkiss pale nilikuwa kazini, kazini naweza kum kiss hata mtoto wangu kama ‘movie’ nayoicheza inaniambia nitembee na mwanangu nitaacha kum kiss? Kwa hiyo pale nilikuwa kazini katika maisha ya kawaida kabisa Raymond mimi ni mdogo wangu, mimi kusema za ukweli huwaga sina tabia za kutoka kimapenzi na wadogo zangu’ alisema Snura.

snura

 eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364