Nahitaji Maombi Yenu Wadau – Ben Selengo
Msanii wa filamu Ben Selengo baada ya kupata ajali ambaya siku ya sikukuu ya Christmas na kulazwa katika Muhimbili, ameruhusiwa na sasa hivi yupo nyumbani.
Muingizaji huyo amedai licha ya kuwa ameruhusiwa kutoka hospital lakini bado afya yake haijakaa sawa na anahitaji maombi.
“Bado nahitaji maombi yenu wadau,” aliandika Ben Instagram “nimetoka Muhimbili nipo home ila kiafya bado,”