Nape Anastahili- Mike Sangu
MWIGIZAJI wa kiume katika tasnia ya filamu Michael Sangu ‘Mike’ amefunguka kwa kuwashangaa watu wanaoponda uteuzi wa waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na michezo Mh. Nape Nnauye kwa kusema kuwa hawamjui vizuri wanatakiwa wafahamu ni mtu makini na anastahili.
Huwezi kuponda tu kwa sababu zako binafsi mimi ninamfahamu kiongozi Nape ni mtu makini na ana uwezo mkubwa sana katika masuala ya uongozi nawashangaa wanaoponda uteuzi wake bila kutambua uwezo wake,”anasema Mike Sangu.
Msanii huyo alisema kuwa mheshimiwa Rais Dr. John Magufuli kutokana na yeye ni mchapakazi hivyo lazima timu yake yote iwe na watu kama yeye na alipoangalia kwa makini akamuona kijana mchapakazi Nape ambaye Mike anaamini kuwa sasa wasanii na wachezaji hawatadhulumiwa tena na wababaishaji.
FC