JB: Chungu cha Tatu ni Filamu Ghali Zaidi
MSANII wa filamu nchini, Jacob Stephen ‘JB’, amesema kuwa filamu yake mpya ya Chungu cha tatu aliyomshirikisha mwanadada Wema Sepetu imetumia gharama kubwa zaidi kuliko filamu zote zilizotengenezwa chini ya kampuni yake ya Jerusalem.
Akizungumza na MTANZANIA juzi, JB alisema ametumia gharama kubwa katika kufanikisha kuitengeneza filamu hiyo.
“Nikisema nitaje gharama iliyotumika na niliyowalipa wasanii nadhani TRA itawafuata, lakini nimetumia gharama kubwa mno naweza kuthubutu kusema imezidi gharama za filamu zangu zote chini ya Jerusalem,” alisema.
Alisema licha ya gharama hizo lakini filamu hiyo inatoa somo kwa wanandoa wengi ambao wana tabia mbalimbali zinazokera hivyo wajifunze na wabadilike kwani kuna mambo ambayo yanachangia kuvunja ndoa.
HEBU FUNGUKA KAMA TAYARI UMESHAITAZAMA CHUNGU CHA TATU