-->

Napewa mabusu kama mtoto wa njiwa – Riyama Ally

Msanii wa Filamu Bongo, Riyama Ally amesema moja ya tabia zinazomchanganya kutoka kwa mume wake, Leo Mysterio ni kupewa mabusu ya kila mara.

Muigizaji huyo ameiambia Times Fm kuwa kitendo kimekuwa kama mfumo wa maisha yao kwa sasa.

“Naona kama ananiibia, mabusu yale, ana mabusu huyu kulamba lambana kama majibwa,” amesema Riyama.

“Nikirudi tu, huko kwenye mapunziko mimi nakula mabusu, nachodolewa chondole tena kama mtoto wa njiwa, unajua tena mzaramo na mibusu,” ameongeza.

Katika hatua nyingi Riyama amesema suala la kuongeza mtoto katika familia yao ni mipango ya Mwenyenzi Mungu hivyo wanavuta subra.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364