Nataka Kuwa Mcha Mungu-Shamsa Ford
Staa wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Shamsa Ford amefunguka kwa kusema kuwa kwa sasa anataka kujikita zaidi kwenye ibada ya kufanya mambo ambayo yanampendeza mwenyezi Mungu.
Mwigizaji huyo ametangaza uwamuzi huyo ikiwa ni miezi michache toka afunge ndoa na mfanyabishara wa maduka ya nguo, Chidi Mapenzi.
Kupitia instagram, Shamsa Ford ameandika
Maisha ya kuendekeza dunia nimeyachoka. Natamani ifike siku kwa kudra za Mwenyezi Mungu nibadilike. Natamani niwe mmoja ya wale watakaopata nafasi ya kwenda peponi pamoja na familia yangu . natamani nifanye IBADA kama ulivyoamua Mwenyezi Mungu. NATAMANI matendo yangu yawe ya kukufurahisha wewe Mwenyezi Mungu ili umauti utaponikuta niwe msafi..G9T MY PEOPLE. ..INSHAAALLAH MWENYEZI MUNGU ATUPE MWISHO MWEMA. .
Mashabiki wake katika mitandao ya kijamii wameonyesha kupendezwa na uwamuzi huo huku wachache wakimuuliza maswali kama ataendelea kufanya tena filamu.