-->

Nay Aamua Kuwachana ‘Wakwaruaji’ wa Bongo Muvi

Star wa Bongo Fleva Nay wa Mitego bado anaendelea kuwapa makavu live wasanii wa Bongo Muvi hasa wakwaruaji wanaosubiri vijana wa bongo fleva wawe juu ndipo watokenao kimapenzi.

NAY23

Akizungumza na Enewz Nay alisema kuwa wadada wenye tabia hizo Bongo Muvi wanajulikana na kuwataja baadhi yao kuwa ni pamoja na Jackilin Wolper, Salma Jabu ”Nisha” na Zuwena Mohamed ”Shilole” na kuongeza kuwa wapo wengi wenye tabia hiyo na kwamba vitu hivyo kwao ni vya kawaida wameshazoea na siku hizi wanaona kama ‘fashion’.

“Mimi nimezungumzia wadada wakwaruaji unajua wakisikia visanii vichipukizi vile wao ndo yaani ndo wanapagawa,wanaviwahi yaani wanawahiana kama sasa hivi kuna kelele zinazoendelea kuna msanii chipukizi anagombewa”

Nay ameendelea kutema cheche “Mimi siwezi kuwalaumu hao vijana kuwa na uhusiano nao unaju inaweza kuwa mtaani siku moja ulikuwa unawishi siku moja kuwa na mtu fulani, halafu ikitokea nafasi kama ile pale aah! Mtu hata upewe ushauri wa dizaini gani mtu ambaye ulikuwa ukimuona kwenye runinga anaingia katika kumi na nane zako mimi siwalaumu japokuwa wanatakiwa kuwa makini”, alisema Nay.

eatv.tv

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364