-->

Ndauka Afungukia Mapenzi, Kampuni Yake!

Leo kwenye safu yetu hii tunaye mwanadada Rose Ndauka ambaye amepotea kidogo kwenye sanaa ya uigizaji kutokana na kubanwa na kazi zake binafsi. Rose ameongea mengi alipokuwa akijibu maswali 10 aliyoulizwa na Mwandishi Wetu Hamida Hassan ndani ya ofisi yake iliyopo Mwenge jijini Dar. Unataka kujua alichofunguka? Fuatilia hapa chini.

ROSE NDAUKA345

Rose Ndauka

Ijumaa: Mambo Rose, mbona kimya sana mama? Umeacha kuigiza au vipi?
Rose: Nipo jamani, sijaacha kuigiza ila kwa sasa kazi zangu binafsi zimenibana. Hata hivyo, mambo yangu yakinyooka nitaendelea na fani. Ujue naongoza kampuni yangu, jambo ambalo siyo rahisi.

Ijumaa: Dah! Hongera sana, kampuni yako inaitwaje na ni nani aliyekupa wazo la kuianzisha?
Rose: Huwezi kuamini ni wazo langu la siku nyingi, niliwahi kuanzisha kampuni nikaibiwa kila kitu, nimejipanga upya na sasa ndiyo kama unavyoona nina hii kampuni inayoitwa Ndauka Entertainment.

Ijumaa: Kwenye kampuni yako umewekeza kama shilingi ngapi?
Rose: Nimetumia kama milioni 100 hivi, kama unavyojua kuanzisha kampuni si mchezo.

Ijumaa: Inasemekana kuna pedeshee anakupa jeuri ya kufanya haya yote, ni kweli?
Rose: Hakuna kitu mwanaume kwenye kampuni yangu, nilijibana kwa muda mrefu na unachokiona hapa ni mali yangu asilimia mia.

Ijumaa: Unaingiza shilingi ngapi kwa siku kwenye kazi moja unayoifanya? Maana ukinitajia milioni mia naziona ni nyingi sana.

Rose: Kwenye hii kampuni nafanya matangazo ambayo kwa moja naweza kulipwa milioni 10 hadi 30. Kwa mfano nimefanya matangazo ya Gepf, Mkapa Foundation na mengine mengi, makubwa na madogo.

Ijumaa: Nasikia unakaa na mama yako mpaka sasa licha ya kuwa na mkwanja wa kukuwezesha kuwa na maisha yako, ni kwa nini?
Rose: Mimi nakaa kwangu Mbezi Beach, Kigogo ndiyo nyumbani kwa mama yangu ila kwa sasa nimemuomba aje niishi naye ili anisaidie kumlea mwanangu.

Ijumaa: Hivi mara ya mwisho kuonana na mzazi mwenzako Malik Bandawe ni lini? Au ndiyo mmeshapotezeana?
Rose: Hatuwezi kupotezeana kwa sababu ya mtoto wetu, yule ni mzazi mwenzangu, linapokuja suala la mtoto tunashirikiana kama kawaida.

Ijumaa: Una mpenzi? Je, umerudi kwenye dini yako ya Kikristo?
Rose: Jamani naomba watu wajue kuwa mimi ni Muislamu. Ninaye mpenzi ambaye ni wa kawaida, si pedeshee ni mfanyakazi kama wengine na ni Muislamu pia.

Ijumaa: Vipi kuhusu mipango ya ndoa na kuongeza mtoto wa pili?
Rose: Bado tunachunguzana na mpenzi wangu, tukiona tunafaa kuwa mke na mume, ndoa itafuata. Kuhusu watoto, nitaongeza kadiri nitakapopata nafasi.

Ijumaa: Kuna madai uliwahi kuwa na matatizo ukamuomba Batuli akupeleke kwa mganga, ulivyofika huko akakugeuzia kibao nyota yako ikachukuliwa, unaliongeleaje hilo?

Rose: Sipendi kuongelea mambo yaliyopita kwa sababu sasa hivi nipo vizuri, namshukuru Mungu nayafurahia maisha.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364