-->

Neno la Shamsa Ford kwa Mumewe Chid Mapenzi

Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford ambaye ni mke wa Chid Mapenzi amefunguka ya moyoni na kusema hata kama dunia nzima itakuwa ikimzomea mumewe, yeye ataendelea kumpenda kwani kitendo hicho hakiwezi kubadilisha mapenzi yake kwake.

Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford akiwa na muwewe Chid Mapenzi

Shamsa Ford amesema hayo kutokana na ukweli kwamba mumewe ni kati ya watu ambao wameitwa Kituo cha Polisi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

“Nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu, huzuni, furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa. Ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya. Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati” alisema Shamsa Ford 

Mbali na hilo Shamsa Ford anasema aliamua kuolewa na Chid Mapenzi kwa kuwa alijua kuwa yeye ndiye mwenye uwezo wa kuwa baba bora kwa watoto wake.

“Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndiyo maana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa. Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani. Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani Inshaallah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi” alisisitiza Shamsa Ford.

eatv.tv

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364