-->

Idris Sultan Asimulia Nafasi Aliyocheza Kwenye Filamu ya Kiumeni

MCHEKESHAJI maarufu Bongo na aliyekuwa mshiriki wa shindano na ‘Big Brother Africa’, Idris Sultan amefunguka amefunguka kwa kuwaonjesha mashabiki wake uhusika aliouvaa kwenye filamu ya ‘Kiumeni’.

Kupitia mtandao wa Instagram, Idris amesimulia kwa kuandika, “Humu ndani nauza madawa kwahiyo nina mpunga wa kumwaga halafu nipo kitaa, demu wangu wa zamani anakuja na mwanaume kumtambulisha kwao na kwa hapa na pale mshkaji anakuja kwangu kapotea, anamlaaaa hamliiiii ??? ?.”

Filamu hiyo imeongozwa na Ernest Napoleon ambaye ni Rais wa D Street Media Group na itaanza kuoneshwa March 17 kwenye majumba ya sinema jijini Dar es Salaam.

Mbali na Idris Sultan filamu hiyo pia imewakutanisha mastaa wa bongo kama Irene Paul, Muhogo Mchungu, Antu Mandoza, Rashid Matumla na wengine.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364