New Music: Harmorapa Aachia Wimbo ‘Kiboko ya Mabishoo’ ft Juma Nature, Awachana WBC
Msanii wa muziki Harmorapa ameachia wimbo wake mpya Kiboko ya Mabishoo akiwa amemshirikisha Juma Nature. Wimbo umeandaliwa na producer T Touchez.
Katika kazi hiyo ambayo tayari imeanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Harmorapa amewachana baadhi ya mastaa akiwemo dansa Mose Iyobo, na watu wengine ambao wamekuwa wakim-‘diss’ kuwa hajui muziki na kusema yeye hajali maneno yao machafu kwani yeye amekuja kutafuta pesa
Bongo5