-->

Nilijinyima Kiasi cha Kuogopa Kula Chips Ili Nisiishiwe- Nisha

diamond267

Msanii wa filamu na mjasiriamali, Salma Jabu aka Nisha amesema mafanikio aliyopata yametokana na kujinyima ambapo amedai ilifikia hatua alikuwa akishinda kwa kula mihogo huku akiogopa kula chipsi pesa zisije zikaisha.

 

Muigizaji huyo ambaye mpaka sasa ana filamu nane ambazo amezitoa kupitia kampuni yake ‘Nisha’s Film Production’, alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa alipitia changamoto nyingi mpaka kupata mafanikio aliyonayo sasa.

“Mimi nilianza na shilingi 50,000 tu pesa yangu ya kwanza ya filamu kulipwa, niliiweka na sikutumia hata shilingi kumi,” alisema Nisha.

“Mimi nilikuwa hata chakula saa nyingine nasema siwezi kula chipsi na kuku, hii acha hata ninunue muhogo mmoja halafu nyingine niweke akiba, ubahili wangu umesaidia. Leo nina biashara, kampuni ya filamu ya mamilioni na nimeajiri watu,” alieleza.

12543367_1692703467611075_1745064822_n

Kwa sasa Nisha ana filamu iitwayo ‘Kiboko Kabisa’ sokoni.

Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364