Nilitarajia Kumuona Raymond Akifanya Vizuri: Madee
Msanii Madee kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu kazi za msanii Raymond ambaye alikuwa Tip Top na sasa yuko WCB.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Madee amesema kuwa alitegemea kumuona Raymond akifanya vizuri, kutokana na jitihada alizokuwa nazo tangu akiwa Tip Top.
“Raymond yuko vizuri anafanya vizuri ni mtu ambaye nimekaa naye najua uwezo wake, ninachokiona nilikitarajia kwamba Raymond atakuwa mtu fulani, Raymond ana kila kitu ambacho msanii anatakiwa awe nacho, mara nyingi huwa naenda nae studio”, alisema Madee.
Pia Madee amezungumzia kuhusu suala la kufanya Hip Hop, na kusema kuwa kila mtu anafanya maisha anayoona yanamfaa, lakini iwapo atatokea mtu akimpa pesa nzuri atafanya Hip Hop.
“Hatulishani kila mtu anafanya maisha yake, ukiniambia mi nichane alafu kila siku unaniletea hela, baridi tu”, alisema Madee.
eatv.tv