-->

Nimejifunza,Nimekoma kwa Wasanii Wenzangu-Steve Nyerere

TENDA wema uende zako ni msemo ambao utumika sana kwa waungwana hili linamshinda mwigizaji na mchekeshaji mahiri Bongo Steven Mengele almaarufu Steve Nyerere baada ya kuonekana kuwa mstari wa mbele katika kujitoa katika matatizo ya wasanii wenzake lakini yeye anapopata matatizo anajikuta akiwa pekee yake na baadhi ya wasanii wachache wakishirikiana.

STEVE345

“Nimejifunza mengi naweza sema kama mtoto nimekomaa kwa wasanii wenzangu ambao ni familia yangu najiona kama wananifanya teja wao badala ya kunijenga wao wananinunulia unga niendelee kuharibika, najitoa sana katika matatizo yao lakini wao wapo nyuma kabiasa,”alisema Steve Nyerere.

Msanii alisema hayo kufuatia msiba wa mama yake mdogo aliyefariki Mikumi na kuhudhuriwa na wasanii wachache pamoja kuwa walitangaziwa wakutane Leaders sehemu ambayo upenda kukutana, Steve ameenda mbali zaidi pale aliposema kuwa akiwahita kwa ajili mipango ya fedha umsumbua kwa kumpigia simu kila muda na ufika sehemu ya tukio mapema bila kuchelewa lakini si msiba.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364