Wema Sepetu Ampongeza Rais Magufuli Kwa Hili
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amefunguka na kumpa hongera Rais Magufuli kwa kuwakuza vijana wengi kiakili na ufahamu kutokana na namna alivyoongoza nchi na kuleta tija kwa watanzania.
Pongezi hizo zinakuja Ikiwa ni takribanmiezi tisa sasa toka Rais Magufuli kutangazwa na kuapishwa kuiongoza Tanzania, msanii wa filamu nchini Wema.
Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema kuwa katika serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli ambayo sera yake ni ‘Hapa kazi tu’ ni lazima vijana wafaye kazi na kuachana na mambo ya maneno maneno yasiyo na msingi katika jamii yetu.
“Serikali ya ‘Hapa kazi tu’ inatakiwa ikukuze kiakili na ufahamu kuwa miaka haiendi nyuma bali inasonga mbele. Dr John Pombe Magufuli asante kwa kutukuza. Huu ni muda wa Kazi tu maneno maneno tuwaachiage watoto wadogo” aliandika Wema Sepetu