Nisha Afunguka Kuacha Skendo za Aina Hii
Muigizaji wa vichekesho kwenye tasnia ya filamu nchini, Salma Jabu a.k.a Nisha Bebee amesherehekea siku yake ya kuzaliwa tarehe 28 kwa kuamua kutembelea Hospital ya Ocean Road kuwaona wagonjwa waliolazwa katika hospital hiyo.
eNewz ambayo ilifanikiwa kufika eneo la tukio ilimkuta Nisha ambaye alisema maisha yake kwa sasa ameamu kuyaelekeza kwa kusaidia watu na siyo kutafuta skendo kama maisha yake ya zamani yalivyo kuwa.
“Siku hizi natumia muda mwingi kusaidia watoto yatima na wagonjwa kwa kuwa nimeamua kuachana na skendo na hata watu ninaokuwa nao mara nyingi ni watu ambao hawapendi skendo tofauti na wale wa awali kwani walikuwa wanavujisha siri zangu” Alisema Nisha.
Pia mwanadada Nisha alitumia fursa hiyo kuwasaidia mahitaji yao ya matibabu na mahitaji madogo madogo ili mradi tu kuhakikisha anamalizia siku yake ya kuzaliwa na wagonjwa ambapo aliamua kujumuika nao katika siku yake hiyo.