-->

Wema Sepetu: Sirudi Tena Dar

Malkia wa filamu Wema Sepetu amelikimbia jiji la Dar es salaam na kuamua kuanzisha makazi mapya mkoani Arusha kama alivyodai mwenyewe.

Wema-Sepetu

Mwigizaji huyo ambaye kwa sasa yupo mkoani Arusha ameonyeshwa kuvutiwa na jiji la Arusha na kuamua kuwarusha roho mashabiki wake kwa kuwaambia kwamba hatarudi tena Dar es salaam.

“My shouger nikimpenda hovyooo, kweli watu tumetoka mbali, huyu ndiye atakayenifanya nihamie Arusha kwakweli,” aliandika Wema katika picha hiyo hapo juu akiwa na rafiki yake.

Kadhi siku zinavyozidi kwenda mrembo huyo anaonyesha kuendelea kuvutiwa mji wa Arusha.

“Nirudie nini Dar mie, kurudi Dar majaliwa, na sirudi Dar ng’o,” aliandika Wema katika ujumbe wake wa pili.

Hata hivyo uwamuzi huyo umepokewa tofauti na baadhi ya mashabiki wake katika mitandao ya kijamii.

Haya ni maoni ya baadhi ya mashabiki wake.


Hopeolivier24

Dar bila Wema Itawezekana kweli? Itakuwa manispaa maana jiji unaliamishia Arusha??

Zai_miss
Kwaiyo ushahamia arusha jamani khaaaa vigoma vyako itakuwaje My mmmh ila umefanya lamaana maana bongo kwa moto arusha Baridi kishezi?????

Theonerealdully
Utarudi tuu. Watu wa dar miji mingine hamuiwezi hekaheka zenu na mafoleni mwayapenda hivyohivyo

Andymsalali
jamn kwann, rudi bhana, tumekuzoea wenyew kukuona dar

Zeyaabdallah
Wema Rudi home coz matatizo hayakimbiwi dadaangu mpenz Wang.sawa Bali unatakiwa uyakabi

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364