Nisha Aongeza Utata Juu ya Mahusiano na Baraka
Msanii wa filamu Nisha Jabu, ametoa upande wake wa maelezo juu ya mahusiano yake na nyota wa muziki Barakah Da Prince, kufuatia kauli ya mwanamuziki huyo wiki iliyopita kukana kuwepo kwa mahusiano ya kimapenzi kati yao.
Nisha amesema kuwa, Baraka ni msanii ambaye ni mchapakazi na anaona mbali, tabia ambayo ni ya aina ya mwanaume ambaye anampenda, akidai kuwa ni marafiki wa karibu ambao hata kulala pamoja kwao ni kitu cha kawaida sana.
Wiki iliyopita, Baraka naye kwa upande wake alikana kuwepo kwa mahusiano ya kimapenzi na Nisha, akidai kuwa kusahau vitu vyake kwa mwigizaji huyo ikiwepo simu, ni vitu ambavyo hutokea na haimaanishi kuwa wana mahusiano.
Utafiti unaonesha kuwa, kuna hisia nzito na ukaribu mkubwa kati ya wasanii hawa wawili, kukiwa na dalili zote za mahusiano mazito ya kimapenzi, licha ya changamoto za hapa na pale, huku wasanii hawa wakikwepa kuweka wazi kinachoendelea kati yao na kuwapa mashabiki sintofahamu kwa makusudi.
EATV.TV