-->

Mzee Majuto Afunguka Kuendelea Kuigiza Mpaka Kifo

Muigizaji wa filamu za vichekesho nchini Amri Athumani maarufu kama ‘Mzee Majuto’ ambaye mwaka jana aliwahi kutangaza kuacha uigizaji na kumrudia Mungu amefunguka na kusema kuwa ataendelea kuigiza mpaka anakufa kwa sababu uigizaji upo kwenye damu.

Akiongea na EATV Mzee Majuto alisema kuwa yeye hawezi kukubali kuona fani inachezewa chezewa na watoto hivyo ataendelea kuigiza mpaka siku atakayokufa kwa sababu uwezo wake ni wa hali ya juu kwenye kuandika na kuigiza.

“Kuigiza kwangu ni kama maradhi vile hivyo sidhani kama naweza kuacha, siwezi kukaa pembeni sanaa ikawa inachezewa na watoto sitaki kabisa nasema hivi mimi nitaendelea kuigiza mpaka nakufa”. Mzee Majuto

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364