-->

Nitagombea Urais wa Tanzania mwaka 2040-Said Fella

Diwani wa kata ya Kilungule wilayani Temeke jijini Dar es salaam Said Fella (CCM ) amesema atagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ifikapo mwaka 2040.

FELLA

Fella ambaye pia ni meneja wa Yamoto band na TMK wanaume fanmily ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na E News ya EATV.

”Kama Mungu akinipa uhai mwaka huo nitakuwa na miaka 60 na nitakuwa nina uelewa wa kutosha na uwezo wa kuweza kuwaongoza watanzania kwa kujali maslahi yao ili kuwawezesha kujikwamua na umaskini” Amesema Fella.

Aidha Fella ametamba kuwa yeye anafanya kazi kwa vitendo ndiyo maana wananchi wa kata yake walimuamini na katika madiwani wote wa Dar es salaam yeye ndiye diwani pekee aliyeshinda kwa asilimia 89% katika uchaguzi mkuu wa October 2015.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364