-->

Nuh Ammwaga Mrithi wa Shilole

MKALI wa Bongo Fleva, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amefunguka kuwa, amemmwaga mpenzi wake aitwaye Erah Erah licha ya kwamba penzi lao lilitawaliwa na mbwembwe nyingi.

mziwanda34

Akipiga stori na paparazi wetu kuhusiana na maendeleo ya penzi lao, Nuh alifunguka kuwa demu huyo haikuwa riziki kwake kwani hakudumu naye baada ya kugundua hamfai na penzi lao limedumu kwa wiki mbili tu.

“Yule nimeshatemana naye, nitampata mkali zaidi yake,” alisema Nuh na kuongeza:
“Nilikuwa na Shilole, nikamuacha, nikampata Erah ambaye naye nimemuacha, naamini nitampata mkali zaidi yao.”
Nuh na Shilole walimwagana hivi karibuni huku kila mmoja akidai hakuwa na amani kwenye uhusiano huo.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364