Nuh: Nimesikitishwa Sana Shilole Kufuta ‘’Tattoo’’ Yangu
Shilole ameifuta ‘tattoo’ ya aliyekuwa mpenzi wake Nuh Mziwanda baada ya kuachana,lakini Nuh hajaifuta na hana mpango kwa sasa wa kuzifuta ‘tattoo’ hizo.
‘’Kiukweli nimesikitika sana hata kama tumeachana mimi mbona sijafuta tattoo zake na sina mpango wa kuzifuta kwa sasa,’’Alisema Nuh.
Hata hivyo Shilole alipoulizwa kuhusiana na alichokisema Nuh alisema kuwa mbona Nuh aliwahi kuwapost mademu zake wapya mara tu baada ya kuachana.
‘’Mimi nimewahi kufuta tattoo kwa sababu yeye alianza kuwapost mademu zake wapya Instagram baada ya kuachana,’’Alisema Shilole.
Cloudsfm