-->

Nyamayao Aibuka, Afafanua Kuhusu Kaole, 2016

Nyota wa filamu Nyamayao kutoka kundi kongwe la Kaole ambalo limetengeneza misingi kwa waigizaji wengi maarufu wa sasa, ameweka wazi kuwa kundi hilo bado lipo.

Nyamayao

Nyamayao

Amesema kundi hilo bado lipo hai ingawa kwa sasa wanaendesha shughuli zao pembeni kama kundi la Kaone, akiwa pia anajipanga kutoka na tamthilia mpya ya muendelezo ambayo taarifa zake zaidi tutazitoa hivi karibuni kupitia hapa hapa EATV.

Nyamayao amesema kuwa, akishirikiana na baadhi ya wasanii wengine kutoka Kaole, wanaendesha shughuli zao sasa kama Kaone wakibadili jina kutokana na misingi ya kisheria wakiwa kama kizazi kipya cha kundi hilo baada ya kizazi cha wasanii wakongwe waanzilishi wa kundi hilo kupita.

Kutoka historia ndefu ya sanaa yake msanii huyo pia ameamua kushare kitu anachokikumbuka zaidi, ikiwa ni kulazimika kukata nywele zake zote ili kuuvaa uhusika aliokuwa akitakiwa katika tamthilia, kitendo ambacho pengine ni kujiongeza ambapo kumefanikisha yeye na sanaa yake kufahamika kwa kiwango ambacho kinaeleweka na asilimia kubwa ya wapenda sanaa hususan ya maigizo.

eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364