Wema na Idris Wafunguka Yote Usioyajua Kuhusu Mimba na Mahusiano Yao
Usiku wa jana Mastaa Wema Sepetu na Idris Sultan walidhibitisha kwa mara ya kwanza kwenye kipindi cha Ala Za Roho na mtangazaji Diva Loveness kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kwamba wana tarajia kupata mtoto wao wa kwanza.
‘’Unajua kuna kipindi nilikuwa siamini nikawa namtuma mdogo wangu akaninunulie ‘pregnancy test’nyingi ili niwe na’test’ kila siku,nilikuwa natakiwa kwenda kufanya ‘process’ ya kusafisha kizazi,nikamwambia daktari wangu kuwa natakiwa kusafisha kizazi ila nikamwambi kuwa nime’miss’ period zangu,akaniambia kabla sijasafisha kizazi nipime kwanza kama nina ujauzito,’’Wema.
‘’Akaniambia kesho yake asubuhi,haja ndogo ya kwanza baada yakuamka nipime, kiukweli kipimo kilikuwa kinaonyesha mstari mmoja mwekundu na mwingine mwekundu lakini kwa mbali …Nikajiuliza ninachokiona au macho yangu nikatoka nikamwamwonyesha mtu mwingine akaniambia nina mimba,nikampigia simu dokta wangu nikamweleza nikamwambia nitaenda na kipimo na yeye akione,’’Wema.
‘’Nilipofika kwa daktari alipokiona aliniambia kuwa nimenasa ujauzito,akaniambia yaani alikuwa akiniwaza kuwa amewazalisha marafiki zangu wengi kwahiyo mimi ningekuwa na mtoto lini,nikamweleza ile ishu ya kusafisha kizazi kwa sababu sijawahi kusafisha katika maisha yangu,akaniambia Mungu ana miujiza yake,akaniambia kesho yake niende nikapime damu,nikaenda nikapimwa kila kitu kilikuwa safi ,akaniambia ninaweza kuanza klinik,’ Wema.
‘’Unajua sijui ni Mungu nilikuwa namwambia mpenzi wangu,Idris kuwa nina mimba lakini nilikuwa sijapima,nilipotoka hospitali nikamwambia mpenzi wangu kuwa nina mimba ili nimuone atasemaje ,’’Wema.
IDRIS ALIJUAJE WEMA ANA UJAUZITO?
‘’ Kuna rafiki yake mmoja alinipigia simu akaniambia kuwa Wema na ujauzito,kipindi hicho nilikuwa nimetoka kukwaruzana na Wema kuhusiana na vitu vilivyokuwa vikiendelea kwenye mitandao ya kijamii,nilivyopokea simu kabla ya kuongea chochote akaniita Baba Kijacho ,nikamuuliza unasemaje ? akaniambia inabidi ufungue akaunt ya mtoto benki…Nikaona kama ananitania ..wakati huo wakati napokea simu nikuwa naendesha gari maeneo ya Mwenge ilikuwa nusu nikanyage matunda ya watu ,’’Idriss.
‘’Unajua mimi sipendi kudanganywa …nikawaza unaweza kuwaambia marafiki zako mara ukaambiwa mimba haipo …baada ya hapo nikaenda kununua vipimo mimi mwenyewe ili nijiridhishe.. nikampigia baby akaniambi yupo nyumbani siku hiyo nililala kwake ….asubuhi yake alienda chooni kipindi hicho anaishi Kijitonyama kwa siri sana nilipomwona anatoka chooni nikienda na kipimo changu…ilichukua muda wa siku tatu kujua kama ni kweli ana mimba bila yeye kujua…,’’Idriss.
‘’Kuna siku alinipigia akaniambia kuwa ana mimba…ikabidi nimwigizie nikamjibu kama sijui….nikasema …Oooh My God…nikamjibu nilikuwa najua siku nyingi nikamuuliza amejipangaje akaniambia yupo poa…Ukweli Wema alikuwa analia kila kuhusu kutosika ujauzito,’’Idris.
UHUSIANO WAO ULIANZIA WAPI?
‘’Kwa mara ya kwanza kumuona Idriss ilikuwa Iview Records kwa Raqie …Ile picha iliyoipost kwenye Instagram nikimuwish happy birthday ndio ilikuwa pich ya kwanza baada ya kufahamiana …tuliongea sana siku hiyo nilienda kufanya photo shoot ya kava la Bab Kubwa …Baada ya miezi kadhaa nikamwona ni mmoja ya washiriki wa shindano la Big Brother ,kipindi hicho nilikuwa naangalia sana Big Brother,kama utakumbuka vizuri kipindi kile nilikuwa napost sana picha zake kwa ajili kuhamasisha watu kumpigia kura ,’’Wema.
‘’Nilivutiwa jinsi alivyokuwa akifanya vituko kwenye lile jumba,sasa kipindi kile alivyokuwa akirudi nyumbani baada ya kuibuka mshindi,nikamtumia sms kwenye Instagram nikamwambia hongera ,akanijibu hey mamy sasa hivi nipo bize kidogo nitakucheki,’I see you’,so alivyopata muda nilimwalika nyumbani kwangu tuliongea sana ,nakumbuka kipindi hicho nilikuwa nipo ‘singo’ nikawa nime weka akili yangu yote kwake,’’Wema.
Cloudsfm.com