Nyerere Kutoa Filamu Kubwa Mwaka Huu
Steve Nyerere amesema baada ya kukaa kimya kwa miaka minne bila kutoa filamu, mwaka 2016 atawapa raha mashabiki wake.
“Nina miaka minne sijatengeneza wala kutoa sinema na si kwamba siuzi,” aliandika kwenye Instagram.
“Kwa mwaka nitakuwa natoa sinema 1 tu ila itakuwa zaidi ya vile tunavyofikiria, ni ubora wa hali ya juu sio kwa mwezi sinema 5, duu ni kumvuruga mteja. Maisha ni kujipanga na kujitambua unataka nini.”