Ommy Dimpoz Afunguka Kuhusu ‘Collabo’ na WCB
Msanii Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Kajiandae’ akiwa na Alikiba amefunguka na kusema hata yeye anaweza kufanya collabo na msanii yoyote yule kutoka WCB.
Ommy Dimpoz alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWz cha (EATV) na kusema kwenye muziki kuna wakati unaweza kupata wimbo ambao unahitaji collaboration na msanii fulani ili uweze kuwa bora zaidi hivyo inapotokea hivyo ni lazima ufanye mawasiliano na msanii huyo ili ufanye naye hata kama yupo WCB au sehemu nyingine.
“Siyo tu Nedy hata mimi naweza kufanya kazi na msanii kutoka WCB siyo tatizo, kwa sababu huu ni muziki pia ni biashara na lazima uangalie wimbo huu naotaka kufanya nikifanya na msanii fulani kutakuwa na hiyo combination nzuri? Kwa hiyo haijalishi kikubwa wote tunafanya muziki na kufanya biashara na kuangalia nikifanya na msanii huyu kazi yangu itakuwa na impact gani kwa hiyo hivyo vitu vyote vinawezekana” alisema Ommy Dimpoz
Mbali na hilo Ommy Dimpoz ameweka wazi kuwa kwa mwaka huu ataachia kazi nne, mbili zikiwa na kazi za kushirikiana na kazi mbili atakuwa amefanya yeye mwenyewe
eatv.tv