Ommy Dimpoz Amshauri Alikiba Amuoe Kidoti
Alikiba na Jokate Mwegelo wanaogelea katika bahari ya huba japo hawataki kualika wageni kujumuika nao – penzi lao ni la faragha.
kadri siku zinavyozidi kwenda, ndivyo mizizi ya uhusiano wao inazidi kumea licha ya kuendelea kuuwekea tinted kuepusha karaha! Licha ya kuwa ya kuwa wachoyo wa kuuweka wazi uhusiano, marafiki zao wa karibu wana access ya kujua kila kinachoendelea.
Mmoja wao ni Ommy Dimpoz ambaye katika ujumbe wa kumpongeza Alikiba kuzaliwa November 29 mwaka huu, alimpa ushauri wa kuhakikisha kuwa anapachika pete kwenye kidole cha chanda cha mpenzi wake – nani mwingine zaidi ya Jojo?
Heri ya Kuzaliwa Mzee Tembo King K @officialalikiba Allaah Akuujalie Afya na Uzima pia Azidi kukufungulia milango ya Heri Ang’oe kabisa ile KoKi ya Baraka yaani Mineema izidi kumwagika Njia iwe Nyeupeeeee ?? pia mwaka huu umuoe yule binti acha kuleta janja janja ukamkimbia ??,” aliandika Ommy.
Ni rahisi kukubali kuwa Ommy alimaanisha binti huyo kuwa ni Kidoti, kutokana na ujumbe wa mrembo huyo kwa Kiba ambao licha ya kuuandika kwa Kifaransa, tafsiri yake ilionesha jinsi anavyomzimia na kwamba ameshindwa kuzuia hisia zake.
Ujumbe huo kwa Kiingereza ulimaanisha:
Baby happy birthday I love you so much,it is paining,I hope that the French has sang you prepare for that, but I want nothing,but the best for you from the bottom of my heart the rest I leave to God for what happens to know that Jojo doesn’t disturb and that am happy to have you as my friend,rest blessed
Bongo5