-->

Bongo Movie Tumekuwa Kama Nyumbu – Gabo

Msanii wa filamu nchini Tanzania ambaye anatajwa kuchukua nafasi ya marehemu Steven Kanumba, Gabo Zigamba, amesema kinachoikwamisha tasnia ya filamu nchini ni kukosa umoja kwa wasanii wa movie kiasi cha kukubali kupelekwa pelekwa kama nyumbu.

gambo02

Gabo ambaye pia ni mmoja kati ya washiriki wanaowania tuzo za EATV, alitoa somo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa akijibu maswali ya wanafunzi wa UDSM, katika kampeni ya ‘Ready To Work’ inayoendeshwa na Benki ya barclays ikiwa na lengo la kukabiliana na tatizo la ajira.

Gabo alisema endapo wasanii wataamua kuwa na umoja wenye nguvu, hakuna kitakachoharibika, na tasnia hiyo itapiga hatua kwa kiasi kikubwa kama ajira rasmi.

“Tasnia ya filamu inasuasua kwa kuwa wasanii tuna umoja wa nyumbu, tuko 20 lakini simba mmoja anatutoa jasho” Amesema Gabo

Akijibu swali kuhusu siri ya mafanikio yake na nani aliyemtoa, Gabo alisema kilichomfikisha hapo ni matumizi mauri ya akili zake na kwamba hakuna mtu yeyote aliyemsaidia huku akiwaasa wasanii wengine kuwa na matumizi mazuri ya akili zao ili kuisukuma mbele tasnia hiyo.

“Nisiwe mnafiki, matumizi mazuri ya akili zangu ndiyo yamenifikisha hapa, siwezi kusema kuna mtu ambaye amenipa mafanikio, katika tasnia ya movie tuna tatizo la matumizi sahihi ya akili, wengi hatujui jinsi ya kutumia akili zetu, tutakapojua kutumia akili zetu tutapiga hatua”

Gabo anawania tuzo hizo kupitia kipengele cha Muigizaji Bora wa Kiume.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364