-->

Uzinduzi wa Filamu ya Siri ya Moyo Watikisa Dar Suncrest Cinema

UZINDUZI wa filamu ya Siri ya moyo iliyotengenezwa na mwigizaji mahiri na mtayarishaji wa filamu Bongo Salum Saleh ‘Man Fizo’ ulifana na kuwa ni kivutio kwa wapenzi wa sinema za kitanzania baada ya watu wengi kujitokeza na kufurahia kazi hiyo ambayo imeshieikisha wasanii nyota katika tasnia ya filamu Swahilihood, sinema hiyo imeonyesha ubora wa kazi za kibongo unavukua kwa kwa kasi.

salum-fizzooo-535-1

Mwanaheri akiwa na wapenzi wa filamu katika uzinduzi wa filamu ya Siri ya Moyo Quality Centre.

Filamu ya Siri ya Moyo ilizinduliwa siku ya Ukimwi Dunia tarehe 1. Dec.2016 katika ukumbi wa sinema uliopo Quality Center ujulikanao kama Suncrest Cineplex Cinema, Filamu hiyo imetengenezwa Tanzania Visiwani (Zanzibar) ikiwashirikisha wasanii chipukizi kwenye Tasnia ya Filamu na baadhi ya wakongwe na wanao fanya vizuri Katika Tasnia yaFilamu Tanzania.

Wasanii nyota kama Amri Athumani (Mzee Majuto), Mwanaheri Afcery Ahmed, Idrasa Makupa ( Kupa), Salum Saleh (Man Fizo) Ambaye pia ni mtayarishaji wa Filamu husika na pia ameshiriki kama mhusika mkuu Filamu hii imetengenezwa kwa kuzingatia viwango vizuri kimataifa na inajenga changamoto kwa wasanii na watayarishaji wengine kuja na kazi zilizo bora zaidi ili kuongeza ushindani katika soko la sanaa kwa namna moja au nyingine.

salum-saleh-man-fizo-89

Man Fizo mtayarishaji wa filamu ya siri ya Moyo

Kampuni ya Steps Entertainment ambaye ndiye msambazaji wa filamu nchini ipo katika kampeni za kuhakikisha kuwa sinema zenye viwango na ubora kuonyeshwa katika kumbi za sinema katika kujenga utamaduni wa watazamaji wa sinema za Kitanzania kuona sinema za kibongo kupitia majumba mbalimbali pia kupitia mtandao wa Afrobox lengo likiwa ni kutumia njia zilizofanikiwa kwa wasambazaji wengine Hollywood na Bollywood.

Aidha mgeni wa heshima katika tamasha hilo lilopewa jina la Bongo Movie Premiere alikuwa ni afisa kutoka Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya kuigiza Benson Mkenda ambaye alisifu utaratibu huo na kushauri pia wadau wengine waunge mfumo huo wa kuonyesha sinema katika majumba ya sinema kwa kufuata Steps pia alimpongeza mtayarishaji wa filamu hiyo Salum saleh (Man Fizo) kwa kutengeneza filamu bora na nzuri.

salum-saleh-man-fizo-89

Msanii anaandika historia kwa sinema yake ya pili kuonyeshwa katika ukumbi huo baada sinema yake ya kwanza kuonyeshwa katika ukumbi huo huo ikiwa ndio sinema ya kwanza ya Kiswahili kuonyeshwa katika ukumbi huo wa Suncrest Cineplex Cinema, jambo ambalo anajivunia kwa kuzidi kupaa badala ya kushuka kisanaa.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364