Ommy Dimpoz: Niko Tayari Kuoa Hata Sasa,Kama Nikipata…
Staa wa Bongo Fleva,Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amesema kuwa yuko tayari kuoa hata sasa hivi kama nikipata mtu sahihi katika maisha yake.
Ommy ameyazungumza hayo wakati akiitambulisha video ya ngoma yake mpya iitwayo ‘Achia Bodi’ kwenye kipindi cha Clouds360 cha Clouds Tv wakati alipoulizwa na mtangazaji kipindi hicho Hudson Kamoga kuwa anatarajia kuoa lini.
“Niko tayari kuoa hata sasa hivi kama nikipata mtu sahihi katika maisha yangu” Ommy Dimpoz.
Miezi ya hivi karibuni msanii huyo alitupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na msichana ambapo picha hizo zilizua maswali kwa mashabiki wake na kuuuliza huenda alikuwa ndiye shemeji yao,lakini hawakupata jibu.
Cloudsfm.com