-->

Uchambuzi wa Bongo Movie Mwaka 2016 Part 1

TAKRIBANI miaka 21 ya Tasnia ya Filamu Tanzania katika ukuaji wake tasnia  imekuwa ikukua kila mwaka na kupata mabadiliko mbalimbali, ndani ya miaka 16 sasa baada ya kuingia katika utayarishaji wa filamu kibiashara kumekuwa na mafanikio na changamoto nyingi, makala ya uchambuzi wa Tasnia ya filamu kwa mwaka huu 2016.

King Majuto akiwa na Msanii mwezake

Historia ya tasnia ya filamu ilianza mwaka 1995 Jijini Tanga pale Mwl. Eli Siagi alipoungungana na watunzi mahiri kama Amri Bawji, Kaini, Jimmy Master, Hassan Master na Bayakub kutengeneza filamu ya kwanza kutengenezwa na wazawa ya Shamba kubwa na kuonyeshwa katika majumba ya sinema karibu nchi nzima. 2003 rasmi wengi wakaingia

Bishara ya filamu imekuwa ikipitia hatua mbalimbali katika ukuaji wake na mwaka huu umekua  mwaka wenye changamoto nyingi zenye kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu, huku njia iliyozoeleka ya uuzaji wa Dvd ikionyesha kupoteza mwelekeo na nafasi pekee kubaki kwa wauzaji wa Dvd kutoka nje yaani tamthilia kutoka Korea na kwingineko.

Kwa upande wa usambazaji.

Tukiwa tumetoka katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kulikuwa changamoto ya soko kudorora hisia zikatawala ikisemekana ni matokeo ya hali ya uchaguzi kuwa ni chanzo, Soko liliendelea kudorora huku mauzo ya DVD kuanza kupungua na hii si kwa sababu ya wezi wa kazi za sanaa bali pia kutoka wauzaji kutafuta bidhaa ambazo watazamaji watazipenda kwa mfano kutafsiri filamu za nje pamoja na Tamthilia mbalimbali.

Makampuni makubwa ya usambazaji katika mwaka huu yamekuwa katika harakati za kubuni mifereji mipya ya usambazaji wa kazi za filamu ikiwa ni pamoja na kuanzishwa hudumu za kiteknolojia za kuuza filamu.

Kampuni kama Steps Entertainment Ltd, iliamua kuhakikisha inaingiza sinem zake kubwa katika Jumba la sinema kwanza na kisha kuitoa na kuipeleka sokoni kwa kiingilia kidogo cha Tshs.5,000 tu, hii imekuwa chachu kwani wasanii wamepata uwanda wa kujidai kutengeneza vichwa vya habari mitandanoni.

Pia kampuni Proin Promotion Ltd, imeweza kutambulisha mfumo wa kuuza sinema kwa kutumai simu kupitia App yao ya proinbox. ilikuja katika wakati ambapo mabadiliko ya Tasnia ya filamu yanakwenda kasi na kuamsha mawazo tofauti kati ya watayarishaji na wasambazaji.

Mbali na hayo pia Kampuni ya usambazaji ya Steps Entertainment iliungana na Television ya Sibuka Maisha pamoja na king’muzi cha Startimes kuleta ubunifu wa hali juu ambapo filamu mbalimbali zinaonyeshwa kupitia chaneli ya sibuka 111. Channeli hii ni ya kulipia hivyo wapenzi wa filamu inawabidi kulipia kwa mwezi na kisha kupata nafasi ya kuwa wa kwanza kuangalia filamu mbalimbali za hapa Tanzania.

Juhudi zote zimekuwa zikifanywa na makampuni mbalimbali ambapo wote wamekuwa na lengo la kupata nafasi ya soko la filamu kwa wateja wanaozidi kugawanyika katika mapenzi ya filamu kiubora, na tukisalia kuzalisha filamu wingi na ubora kwa maana uzalishaji mbovu na kukosekana kwa maudhui simulizi.

Katika kuleta hali ya kiushindani pia Steps Entertainment Iliona mwanya kuwa kuhakikisha kuwa inapata nafasi katika soko la kimtandao ambapo imejiunga  pamoja na App ya Afrobox kuweza kuwapa wapenzi wa sinema za hapa nyumbani urahisi wa kuzipata.

Hata utabaini kuwa mlishaji mkuu katika vyombo vya habari yaani Televisheni ni Kampuni ya Steps kwa maana asilimia kubwa kwa Runinga zenye vipindi vya filamu za nyumbani nyingi zinaonyesha kazi za kampuni hiyo jambo ambalo kiushindani kuna wateja wanaweza kuumia kwa kurudia filamu katika Chaneli yake.

Changamoto katika soko la filamu zimekuwa ni nyingi si katika usambazaji tu bali pia katika utayarishaji hasa uandishi,  Filamu nyingi zimekuwa haziafuta misingi bora ya kiuandishi  na hivyo kuleta hali tata katika umaliziaji wa sinema ili wazo ama maudhui yake kuifikia hadhira na kueleweka kirahisi.

Dkt. Mona Mwakalinga akiwa na Mwl.Issa naye ni mwezeshaji ktk Semina za wadau wa filamu

Lakini jambo lingine muhimu kuliko yote ni suala la Ubunifu kushuka kwani kila filamu unayokutana nayo mtaani itakuwa sura hizi King Majuto, Riyama Ally, Hemed Suleiman, Bi. Mwenda, Bi. Hindu, Mzee Msisiri,Jengua, Hashim Kambi na wengineo kiasi cha kuona jinsi maudhui yakijirudia kwa kila kazi Riyama kwa sasa si yule wa Fungu la Kukosa.

Unapokutana naye tu jiandae kuchambwa hata kama itakuwa ni scene ya ugonjwa au msiba inaonekana lazima iwe hivyo coz alifanikiwa, lakini hilo halipo kwa waigizaji tu hata watayarishaji nao ubunifu umekimbia ikitokea sinema moja tu ikifanya vizuri basi kila ijayo ni Vigodoro tu, tunahitaji kukimbia zaidi ya  sasa.

Bodi ya filamu na wadau wengine wameweka kipaumbele katika hili na hapo awali tuliona watu kama Dkt. Monna Mwakalinga kwa kushirikiana wadau wengine waliweza kuandaa semina mbalimbali za kufunda Watayarishaji wa filamu ingawa bado mwamko umekuwa ni mdogo.

Jitiada hizi ni katika kuhakikisha hali hii ya soko iweze kuokolewa kwa kupata sinema zenye ubora, kama zile unazoziona, pia Bodi ya Filamu kwa kuliona hilo wamekuwa msaada mkubwa kwa kuanzisha program maalum ya kuwajengea uwezo wadau wa filamu Tanzania na tayari mikoa kama Morogoro, Mwanza na Mara imefaidika na Program hiyo muhimu.

Kama ilivyo kawaida kwa jambo lolote lifanyikalo Bongo neno changamoto ni chachu na huwa halikosekani basi tunapoongelea suala la Warsha za kuwajengea uwezo watengeneza filamu ni ushiriki mdogo kwa wale wasanii wenye majina ambao wanaamini kipaji kuliko Elimu kitu kinachowakosesha Weledi kwa kazi wafanyayo.

Tumeona harakati ambazo zimefanyika katika Tasnia ya filamu kwa 2016, Tunaamini kwamba changamoto zinaleta mabadiliko Chanya Je ni mabadiliko gani yanatufaa au ni yapi ambayo yataleta faida kwa mwaka 2017?, au kuna manufaa katika haya mabadiliko?!.

Mwaka 2017 ni wa mabadiliko sana hasa kwa FC Tutaendele kujadili harakati za Tasnia ya filamu katika nyanja za mbalimbali kwa Waigizaji, Utayarishaji wa Tamthiliya za Television,Vikundi vya sanaa na nyingine nyingi. Endelea kufutailia makala hizi. Kupitia www.filamucentral.co.tz

Imeandikwa na Staford Kihore.

Kuhaririwa na Myovela Mfwaisa.

Central Filamu

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364