-->

Picha: Mamia ya Wakazi wa Jiji la Mbeya Wamzika Kinyambe

MBEYA: MAMIA ya wakazi ya jiji la Mbeya wamemzika aliyekuwa msanii wa vichekesho James Petro Nsemwa (30) maarufu kama Kinyambe ambaye alifariki dunia jumatano ya wiki hii mkoani Mbeya, katika makaburi ya Hayombe Uyole Igawilo mkoani Mbeya.

KIYEMBA

Msururu wa wakazi wa jiji la Mbeya pamoja na magari ulitembea kutoka nyumbani kwa wazazi eneo la makondeko mtaa wa mtakuja kata ya Igawilo kuelekea makaburi ya bonde la uyole kwa umbali kilometa tatu na nusu.

Pia baadhi ya wasanii kutoka Dar es Salaam wakiongozwa na kitale waliudhuria mazishi ya msanii mwenzao ingawa hapakuwepo na uwakilishi wa viongozi ngazi ya mkoa uliyofika mazishini.

KIYEMBE298

Msiba huo uliosimamisha shughuli mbalimbali kwa muda ili kupisha msururu wa watu na magari ambao ulikuwa ukielekea makaburini yaliyopo eneo la Nsalaga.

Baba wa marehemu, mzee Lugendelo Nsemwa, amesema kuwa akiwa nyumbani kwake Uyole, kuwa mwanaye ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa uchekeshaji, alianza kuumwa tangu Juni mwaka jana, ambapo moyo, tumbo na miguu ilikuwa imejaa maji pamoja na pafu la kushoto.

KIYEMBE92

Alisema tatizo hilo lilipelekea mapafu yake kushindwa kufanya kazi sawasawa.

“Kwa kipindi kirefu alikuwa amelazwa katika hospitali mbalimbali kama vile Uyole, Ifisi, Rufaa na hospitali ya mkoa wa mbeya, hali yake ilibadilika, alizidiwa na kupoteza fahamu, na bahati mbaya Jumatano saa 3 usiku akafariki dunia,” alisema mzazi huyo.

KIYEMBE90

Komediani huyo aliyetamba kwa kubadilisha sura na sauti yake katika filamu za uchekeshaji nchini, James Petro Nsemwa a.k.a Kinyembealizaliwa tarehe 19.09.1985 katika kijiji cha Mahanji- Matamba.
 KIYEMBE01
Kinyambe hakuwa na kiwango kikubwa cha elimu ambapo aliishia kidato cha pili mwaka 1999, kisha akajiunga na masomo ya sanaa katika mkoa wa Tanga kwa mwaka miwili.
mke-wa-kinyambe

Mke wa Marehemu Kinyambe

Marehemu alikuwa msanii wa kuigiza na kuchekesha ambaye alizunguka mikoa karibu yote yaTanzania na nchi za nje kama vile Malawi, Msumbuji na Zambia.
KIYEMBE00
Source: SIMBAYABLOG

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364