-->

Picha za Wema na Ommy Wakiwa Chumbani Zawa Gumzo

DAR ES SALAAM: LICHA ya tetesi kuzagaa kuwa amerudiana na mpenzi wake, Idris Sultan, mtoto mzuri Bongo Muvi, Wema Sepetu kwa mara nyingine ametengeneza habari, amedaiwa bado anaendeleza uhusiano wa siri na staa wa Bongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, Risasi Jumamosi limepewa mchapo.

WEMA-NA-DIMPOZ-3

PICHA ZADHIHIRISHA
Hiyo imedhihirika hivi karibuni baada ya kuvuja kwa picha mpya za wawili hao wakiwa chumbani katika mapozi ya kimahaba huku wamevaa mavazi ya kulalia .
Picha moja wapo ilimuonesha Dimpoz akiwa amemwekea miguu Wema mgongoni huku nyingine akiwa ameegesha mkono kwenye kalio kitendo ambacho kinaleta tafsiri ya mtu na mtu wake.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kilicho karibu na Dimpoz, kimepenyeza habari kuwa, licha ya Wema kupitia uhusiano tofauti, Dimpoz amekuwa akiendelea ‘kujiweka’ kwa siri jambo ambalo watu wengi hawalitambui.
“Mbona kitambo tu, Dimpoz amejiweka kwake kiulaini, sema wenyewe wanafanya mambo hayo kwa siri. Si mnajua Dimpoz si mtu wa kutangazatangaza mambo yake na ndiyo maana hadi Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki) akafikia hatua ya kumhisi vibaya hadi kumuimba kwenye wimbo wake,” kilisema chanzo.

WEMA-NA-DIMPOZ-32

MAZINGIRA YA TUKIO
Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, picha hizo walipiga wenyewe chumbani, nyumbani kwa Dimpoz,  Kinondoni jijini Dar hivyo zilibaki katika simu ya Dimpoz ndipo chanzo hicho kilipozikwapua na kuzituma kwa paparazi wetu.
“Bwana nakupa lakini msinitaje huko, nyie kamilisheni mambo yenu lakini habari ndiyo hiyo; Dimpoz na Wema ni kapo ya kimyakimya maana wenyewe hawataki kuanika mambo yao,” kilisema chanzo hicho.

DIMPOZ HUYU HAPA
Baada ya kumkosa Wema, mwanahabari wetu alimtafuta Dimpoz ambaye alikiri kuwa picha hizo zilikwapuliwa kutoka kwenye simu yake lakini akadai hawana uhusiano wa kimapenzi.
“Hizo picha nazijua, nakumbuka tulipiga hapahapa Dar. Ilikuwa ni hotelini na si nyumbani kama huyo mtu alivyowaambia lakini kitu cha msingi unachopaswa kujua, Wema ni mshikaji wangu wa karibu na hakuna kitu kingine zaidi ya ushikaji. Kuna mtu itakuwa kanifanyia umafia kwenye simu lakini nitadili naye lazima nitamjua tu,” alisema Dimpoz.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364