Picha: Wolper na Harmonize Mahaba Niue
Couple inayokuja kwa kasi Bongo kati ya staa wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper na mwanamuziki anayekimbiza katika Bongo Fleva, Harmonize imezidi ku-make headlines katika mitandao ya kijamii.
Wawili hao walianza kwa siri lakini kwa sasa wameamua kuweka mambo hadharani bila kupepesa macho na kuudhihirishia umma kuwa kwa sasa ni wapenzi na hakuna kificho tena.
Katika kuonyesha kuwa ni wapenzi, majuzi wawili hao waliamua kuonyeshana mahaba live bila kujali watu waliokuwa katika sherehe ya kutimiza mwaka mmoja wa kuzaliwa mtoto wa Aunty Ezekiel na Moses Iyobo aitwaye Coolie kama inanyoonekana katika video hii hapa chini.