-->

JB Adai Alizitolea Nje Ofa Tatu za Movie za Kinaijeria

JB si msanii anayezuzuka na filamu za Kinaijeria ndio maana amesema ameshazitolea nje ofa tatu za kuigiza filamu za Kinaijeria.

JB8990

“Natoboa siri ambayo watu hawaijui, nimekataa script zaidi ya tatu Nigeria kwenda kuact kwasababu hazinilipi,” muigizaji huyo aliiambia 255 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Naapa mbele ya Mungu ukitaka nitakuonesha, zipo. Sababu ni moja tu fedha iliyolipwa ni ndogo wakisema kwamba tunakutengeneza ili wakujue. Siko tayari kutengenezwa sasa hivi, mimi ninachotaka ni hela. Filamu yangu moja hapa nikiuza napata hela nzuri sana,” ameongeza.

JB amesema international anayoitaka yeye si kwenda kufanya filamu Nigeria bali kutengeneza filamu ambayo itaoneshwa kwenye majumba ya sinema duniani.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364