-->

Picha:Mwili wa Samuel Sitta Ulivyopokelewa Uwanja wa Ndege Dar

Mwili  wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta umewasili jioni hii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ukitokea nchini  Ujerumani ambako alikuwa akitibiwa hadi mauti yalipomfika.

Mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege, mwili wa Marehemu Sitta utapelekwa nyumbani kwake Msasani, Dar es Salaam.

mwili-wa-sitta-1

mwili-wa-sitta-4

mwili-wa-sitta-3 mwili-wa-sitta-5

 

Taarifa zilizotolewa na msemaji wa familia ya marehemu, Gerald Mongella, zinasema:

Kesho, Ijumaa saa tatu asubuhi kutakuwa na ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Sitta itakayofanyika katika Viwanja vya Karimjee ambako ndugu, jamaa, marafiki na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam watapata fursa ya kumuaga.

Baadaye mwili wa Sitta utasafirishwa hadi mkoani Dodoma ambako utaagwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kisha kusafirishwa kwenda Urambo mkoani Tabora kwa mazishi yatakayofanyika Jumamosi.

Marehemu Sitta alifariki dunia Novemba 07 mwaka huu katika Hospitali ya Technal University iliyopo nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya saratani ya tezi dume.

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI. AMEN

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364