-->

Prof. Jay Ameanza Kunielewa- Steve Nyerere

Mchekeshaji na muigizaji wa bongo ‘movie’ Steve Nyerere amefunguka mengine mapya kwa kudai hana haja tena ya kuendelea kutukanana na watu wasiojielewa kwa kuwa ameshajitokeza mkombozi wake mwenye akili na kutambua kilio chake kinamaana gani.

Mchekeshaji Steve Nyerere

Steve amesema hayo baada ya kile kinachoaminika kuwa Mbunge wa Mikumi, Mhe. Joseph Haule kusimama mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwatetea wasanii kwa ujumla kwa kuitaka serikali kuwekeza fedha za kutosha katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili wizara hiyo iweze kuwekeza katika sanaa na kuacha kuwatumia wasanii katika chaguzi na kampeni mbalimbali kisha kuwaacha kama makarai ya kujengea maghorofa na vitu vingine lakini nyumba ikakamilika yanawekwa uvunguni hayatakiwi wala kuthaminiwa hata kuonekana kwa wageni wa aina yoyote wale.

“Mwenye akili anaanza kuelewa nalilia nini kwenye sanaa yetu..Sina haja ya kutukanana ni wajinga wanao tukana. Ukweli unadumu kuliko kitu chochote, ukweli huzaa amani..Asante Mhe. Haule kwa kuongea ukweli”. Alisema Steve kupitia ukurasa wake wa instagram

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364