Rachel, Tunda Waungana na Akina Wema, TID Police Central -Dar
Video Queen maarufu hapa Bongo, Tunda pamoja na msanii wa Bongo Fleva, Winfrida Josephat ‘Rachel’ wameripoti leo katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazowakabili za kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.
Tunda na Rachel wanaungana na wasanii wengine waliohojiwa na kushikiliwa kituoni hapo Ijumaa iliyopita ambao ni Wema Sepetu ‘Madame’, Khalid Mohamed ‘TID’, Babu wa Kitaa, Nyandu Tozi.
Wasanii wengine ambao walitajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na hawajaripoti kituoni hapo ni pamoja na Kher Samir ‘Mr. Blue’, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’, Vanesa Mdee ‘Vee Money’ pamoja.
Chanzo:GPL