-->

Sakata la ‘Unga’: Makonda Ametoa Siku 10 kwa Wahusika Kujisalimisha

LEO Jumatatu, Februari 6, 2016, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa na Kamanda Sirro katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam amezungumza na wanahabari kuhusu oparesheni ya kusaka wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya kwa mkoa wake.

Mambo  aliyoyasema Paul Makonda leo ni kutoa siku kumi kuanzia kesho February 7, 2017 kwa Wenyeviti wa mtaa, Wazazi na Watumiaji na Wafanyabiashara.

==>Natoa siku 10 kwa kila Mwenyekiti wa Mtaa kwenye mitaa yote Dar es Salaam kutoa taarifa za mtaa wake juu ya dawa za kulevya.

==>Natoa siku 10 kuanzia kesho kwa Wazazi, kama wewe ni mzazi unaishi na mtoto anatumia dawa za kulevya na unaishi nae, njoo utoe taarifa….. tukikukamata baada ya siku kumi na mwanao anahusika tutaamini na wewe ulikua sehemu ya kumfanya mtoto wako atumie dawa za kulevya.

==>Natoa siku 10 kwa Wafanyabiashara na Watumiaji wa dawa za kulevya, waje wenyewe Polisi kwa kamishna, kama umekua ukifanya biashara ya dawa za kulevya na umeacha njoo Polisi, nguvu tunayo, uwezo tunao…. hakuna kiunga tutashindwa kufika, hizi kelele nyingine zinatupa hamasa

Chanzo: GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364