-->

Rais Magufuli Azungumzia Swala la Madawa ya Kulevya, Asema si Kazi ya Makonda Peke Yake

Rais John Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohusika na Dawa za Kulevya. Asema si kazi ya Makonda peke yake.

Rais Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu

Rais Magufuli amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina yao.

Rais pia amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu kwa kuwasimamisha kazi askari 12 ili kupisha uchunguzi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za dawa za kulevya.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo Ikulu jijini hapa wakati wa sherehe za kumuapisha Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo.

Zaidi Tazama Video hii

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364