-->

Rais Magufuli Ampigia Simu MwanaFA na Kumpongeza

Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli ni shabiki wa muziki wa Hamis Mwinyijuma maarufu kwa jina la MwanaFA, hilo limewekwa wazi na msanii mwenyewe.

Rais Magufuli ameamua kuweka hisia zake hizo wazi kwa kumpigia simu msanii huyo wa Bongo Fleva na kumfikishia ujumbe kuwa yeye ni msikilizaji mzuri wa wimbo wake wa Dume Suruali.

Katika wimbo huo ambao rais anaupenda, MwanaFA amemshirikisha mwanadada Vanessa Mdee na video yake ikiwa imerekodia Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, msanii huyo ameandika:“Nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais @MagufuliJP kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa #DumeSuruali,” ametweet Mwana FA.

Baadaye akanogesha kwa kuandika: “Utoe heRa kwani ina tv ndani?” (in his voice) ??…,”


Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364