-->

VIDEO: Alichokisema Rose Ndauka Kuhusu Madai ya Bongo Movie Kufa

Staa mrembo kutoka Bongo Movie, Rose Ndauka amelifungukia swala na madai ya kuwa bongo movie imekufa kwa kueleza kuwa bongo movie haijafa kwa sababu wapo wasanii wanafanya kazi nzuri na kuwa  tatizo jamaii haitaki kuwapokea wasanii wapya.

Akiongea na Ayo TV Entertainment, Rose Ndauka  alifun guka kuwa  anayesema Bongomovie imekufa anasambaza habari za upotoshaji tu kwa kuwa hakuna ukweli wowote.

”Tatizo ni kwamba, jamii haitaki kwanza kuwapokea wasanii wapya waliokuwepo. Kwa hiyo, kama tunaongelea Bongo movie kama kikundi cha watu, hapo sawa, lakini kama tunaongelea Bongo movie kama tasnia ya filamu Tanzania, basi Bongo movie haijakufa, kwa sababu bado kuna watu wanafanya vizuri. Kwa nini msiwaongelee watu kama Ernest wa Going Bongo, amefanya vizuri.” Rose Ndauka.  

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364