-->

Rammy Galis: Kucheza Series Inalipa Kuliko Bongo Movie

Hivi karibuni nilipata chance ya kupiga stori na mwigizaji wa Bongo Movie Rammy Galis ambaye pia anaonekana kila wiki kupitia tamthilia ya Kitanzania ‘HUBA’ inayorushwa exclusively kupitia channel ya Maisha Magic Bongo kwenye DSTV.

Rammy Galis

Ukiachana na yeye kufanana sana na marehmu Steven Kanumba, Rammy Galis ni mtu mmoja poa sana na anayejitambua. Nilibahatika kukaa na kupiga nae stori chache na kufanikiwa kumuuliza msanii huyo vitu vingi ikiwemo utofauti wa kucheza Bongo Movie na Tamthilia za TV, kipi kinalipa zaidi kati ya viwili hivyo na ilikuaje kuaje mpaka akapata shavu la kucheza tamthilia ya ‘HUBA’ ambayo kwa sasa ni miongoni mwa tamthilia za kiswahili zenye ubora wa hali ya juu wa picha.

Production wise wapo advanced sana kupitia camera zao na drone shots… wana vitu vingi vizuri which is very good… ” – Rammy Galis.

Hivi ni baadhi ya vitu alivyoniambia:

Sababu Zilizompelekea Kucheza Tamthilia Ya HUBA:

Niliamua kufanya series kutokana na maslahi ya kazi. Stori ya HUBA ni ya Wakenya waliomua kufocus kuifanyia Tanzania na walivyokuja na list ya wasanii waliotaka kufanya nao kazi niliombwa kuwa main character wa series hiyo, lakini sababu nyingine iliyonisukuma kucheza series hii ni baada ya kuona ‘Oh. Kumbe hata DSTV wanaziona kazi zangu’ nikaona it’s good na ilikuwa na maslahi mazuri na pia DSTV ni sehemu ya kutengeneza coverage kubwa kwasababu hii ni series inayoonekana Africa nzima.

Tofauti Kati Ya Kucheza Bongo Movie Na Series (Tamthilia za TV):

Kuna tofauti kubwa sana. Kwanza nilivyokuwa nafanya ile series walikuwa na hospitality kubwa na walikuwa wanajua kukujali sana, pia maslahi sio madogo ni makubwa tofauti na mtu aliyeku-hire kufanya Bongo Movie. Pili production wise wapo advanced, wamejitahidi sana kupitia camera zao na drone shots, vitu kibao yani which is very good na naona itasaidia kuboost tasnia ya uigizaji Tanzania.

Kipi Kinalipa Zaidi Kati Ya Bongo Movie Na Series:

Series ofcourse inalipa zaidi lakini intagemea unafanya kazi na nani. Kwenye series hii sijaingia cost kubwa ya kuandaa watu, sijaingia cost kubwa ya kwenda kushoot na watu… mimi nimeitwa nimefanya kazi inayoruka, kazi yangu ilikuwa kuvaa, kusoma script na kucheza…so inategemea unafanya kazi na nani na budget yao ya production ipoje.

Juu Ya Mipango Yake Ya Sasa na ya Karibuni :

What next ni premier ya movie niliyoifanya Nigeria ‘Red Flag’… licha ya hiyo nina movie ninayoshoot inaitwa ‘The Secret Job’ bado haijaisha, nasubiria support kutoka producer mmoja wa Nigeria. Pia nina movie mbili nilizozifanya Nigeria, Mungu akipenda nitazipremier mwezi wa 6 Nigeria na pia tutaangalia uwezekano wa kuipremiere movie hiyo na hapa Tanzania.

Kikubwa cha kufahamu kuhusu movie mpya ya Rammy Galis ‘Red Flag’ ni kwamba official premier ya movie hiyo itafanyika Mwezi ujao wa April (tarehe bado kutajwa) kwenye kumbi za Sinema Mlimani City na kuna uwezekano mkubwa wa filamu hiyo kupata airtime ya kuonyeshwa kwenye kumbi hizo za Century Cinemax.

Kwa wale wapenzi na wafuatiliaji makini wa tamthilia ya ‘HUBA’ mkae mkao wa kupokea misimu endelevu, ikiwemo msimu wa nne, tano, sita na pengine wa saba… ningependa kuwatonya kile kinachoenda kutokea mbeleni ila nimeombwa nisiharibu uhondo wa stori na mategemeo ya watu kwahiyo mtaniwia radhi.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364