Ray Awaasa Vijana Juu ya Hili
Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kusema kuwa yeye furaha yake ni kuona vijana wenzake wakifanikiwa na kupiga hatua kimaendeleo.
Ray Kigosi amewaasa vijana wenzake kuwa wasikae wakategemea kuwa viongozi wa siasa wanaweza kuja kuwabadilishia maisha yao bali amewataka kuwa na jitihada binafsi kwani huo ndiyo msingi mkubwa wa mustakabali wa maisha yao.
“Furaha yangu ni kuona kijana mwenzangu ukifanikiwa na kupiga hatua kimaendeleo, pambana achana na mambo yasiyo na msingi ukitaka kufanikiwa katika ndoto zako fanya vitu vigumu kufanyika. Fanya kitu ambacho mwingine hawezi kufanya, hakuna kiongozi yeyote wa nchi atakayekuja kuyabadilisha maisha yako isipokuwa ni jitihada zako mwenyewe huo ndio msingi mkubwa wa mustakabali wa maisha yako.”
eatv.tv