-->

Ray Baada ya Kukimbiza na Maji Sasa Anakimbiza Filamu ya Tajiri Mfupi!

MUONGOZAJI,mtayarishaji na mwigizaji wa filamu  Vincent Kigosi ‘The Greatest’ Mzee wa Maji akiendelea kutikisa na unywaji wa maji sasa ameibuka na filamu yake kali na ya kusisimua ya Tajiri Mfupi ambayo ipo madukani na inatembea kama karanga kila mtu anataka kujua Mzee wa Maji kafanya balaa gani humo!

ray34

anasema kuwa filamu ya Tajiri Mfupi ni sinema ya kipekee kabisa kutengenezwa Bongo hivyo kila atakayenunua lazima afurahie kazi hiyo ambayo inaburudisha na kufundisha pia.

“Ukisema Ray na kazi zake hakuna asiyejua umakini wangu sasa hapa nakuja na filamu ya Tajiri mfupi sinema bora kabisa kwa mwaka huu, nimekuja kivingine natoa nafasi kwa msanii mdogo kabisa katika tasnia,”anasema Ray.

Filamu ya Tajiri mfupi imewashirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu Swahilihood kama Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Hussein Chodo, Idrissa Makupa ‘Kupa’, Muhogo Mchungu, Ray na wasanii wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo na inasambazwa na Steps Entertainment.

FC

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364