-->

Ray C Ataka Kujiua Mara 10

MWANAMUZIKI ambaye miaka kadhaa iliyopita alipotea kwenye anga la muziki baada ya kujitumbukiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amefunguka jinsi alivyotaka kujiua zaidi ya mara 10 kutokana na kujichukia.

Akizungumza na Wikienda katika mahojiano maalum wikiendi iliyopita, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kuwa, alifikia uamuzi huo mara kwa mara baada ya kujichukia kupita kiasi huku akiona kuwa hana thamani tena duniani wala hajui atatokaje kwenye dimbwi alilojiingiza akiwa bado msichana mdogo.

“Kujiua kwangu lilikuwa ni wazo la mara kwa mara, inaweza ikawa hata zaidi ya mara kumi kutokana na kukata tamaa kabisa ya maisha huku nikijitazama nilivyokuwa msichana mwenye ndoto nyingi lakini nateketea nikijiona,” alisema Ray C.

Mwanamuziki huyo ambaye amerejea kwenye gemu kwa kishindo alisema kuwa, nia ya kujitoa uhai ilikuwa ikitokana hasa na kuamini kwamba hawezi tena kujinasua sehemu aliyokwama kutokana na kujaa vizingiti vya kushindwa hivyo kufikiria hakuna njia nyingine zaidi ya kifo.

“Kuna wakati nilikata kabisa tamaa kuwa hakuna njia nyingine ya kunifanya nipumzike na tabu niliyokuwa nikipata zaidi ya kujitoa uhai ambao kwangu haukuwa na thamani na wala sikuwa ninajipenda tena hata kidogo,” alisema Ray C ambaye anatamba na wimbo wake mpya wa Unanimaliza.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364