Baada ya Ndoa ya Pili Flora Afunguka Haya
Msanii wa nyimbo za injili Tanzania Flora ambaye alikuwa mke wa Emmanuel Mbasha jana amefanikiwa kufunga ndoa yake ya pili na kijana Daudi Kusekwa baada ya ile ya kwanza kuvunjika na kupeana talaka na Emmanuel Mbasha.
Baaada ya kufunga ndoa hiyo jana Flora alisema yeye ana amani ya moyo licha ya watu kuendelea kusema maneno juu yake na maisha yake.
Flora amesema yeye hajali jinsi gani watu wanamtazama kutokana na maamuzi yake hayo bali yeye anachoangalia ni furaha yake na kusema kwa sasa yeye ana amani na furaha ya moyoni na hayo maisha mapya, ambayo ameamua kuwa nayo.
“Unapofanya maamuzi na kuhisi kwamba unaamani na uko sawa sawa just do it, kwa sababu wanadamu tumeubwa kusema hata huyo ambaye umekaa naye karibu hapo anaweza kuonyesha kukufurahia, hata mtu ambayo yupo karibu na wewe anaweza kuwa anakuchekea ukajua kama ni rafiki yako kumbe ni adui yako mkubwa, kwa hiyo unapokuwa unataka kufanya jambo na kuhisi una amani ya moyo bora ufanye maana wanadamu hawachoki kuzungumza” alisema Flora
Flora Henry jana jijini Mwanza alifunga ndoa yake ya pili na kijana anayefahamika kwa jina la Daudi Kusekwa ambaye ni mwenyeji wa jiji la Mwanza na baada ya ndoa hiyo Mume wa Flora, Daudi Kusekwa alifunguka na kuwataka Watanzania sasa watambue kuwa Flora si mke wa mtu mwingine bali ni mke wake yeye halali
eatv.tv