-->

Roma Mkatoliki Anena Jambo

Roma Mkatoliki akiwa na mkewe Nancy (Kushoto) katika Ibada siku ya Jumapili ya jana.

Msanii Roma Mkatoliki ambaye alikuwa akiuguza majeraha baada ya kutekwa na kuumizwa amefunguka na kusema hali yake inaendelea vyema na ameamua kutoka rasmi sehemu aliyokuwepo kwa kufanya misa ya shukrani jana na baada ya hapo aendelee na maisha yake.

Roma Mkatoliki ambaye jana aliambatana na mkewe na kufanya Ibada ya misa takatifu ya shukrani kwa Mungu katika kanisa la St. Peters Oysterbay kumshukuru Mungu kuwavusha katika kipindi kigumu na baada ya hapo Roma amesema sasa anaweza kuendelea na maisha yake ya kawaida.
Msanii huyo amedai kuwa ngoma zake nyingi alizokuwa amezifanya zote zimepotea baada ya vifaa vya studio kuchukuliwa na watekaji, Roma pia amesema kwa sasa anawaacha Watanzania wawe na shauku hivyo hivyo kutaka kujua akirudi atarudi na ngoma gani.
Mbali na hilo Roma Mkatoliki amesema kwa sasa yupo tayari kufanya show ili maisha yake yaweze kuendelea kama kawaida maana katika kipindi chote yupo ndani hakuna msaada wowote ambao wamepata kutoka kwa viongozi wa serikali, hivyo ameamua kuendelea na kazi ili kuendesha maisha yake ya kila siku, huku akiomba kwa yoyote ambaye atagushwa kusaidia studio yao ya Tongwe Records iweze kurudi kama zamani ili waweze kuendelea na kazi zao kama zamani.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364